Siku za mwizi ni arobaini

Na mchumba wangu amenitoroka

Alinishika nikionja tunda marufuku

Midomo yangu na asali

(Chorus)

Amepotea njiani

Namtafuta simwoni

Ameniacha? La siamini

Mola nipe mabawa nimtafute majangwani

Mola nipe mabawa

 

Nimeenda mahali yote tuliyoyapenda

Simwoni na mimi sijulikani

Naitwa mjinga naambiwa, ‘Umepoteza malika.

Na umerudi utumwa.’

 

(Chorus)