Tulifunga macho kuomba

Tuliibiwa ardhi

Bendera ya Mungu ilipeperuka

Mwafrika akikaa kwa imani

Cheupe kilijiuza

Cheusi kilifukuzwa

Tuliambiwa, ‘Imbeni alleluia,

Fungeni macho imbeni.’

 

(Chorus)

Tumegongwa tumeamka

Tumekanyagwa tumejitoa

Tumelazwa tumesimama heye!

Tumebanwa tumeepuka

Kusulubiwa tumeshuka

Tumeuawa tumefufuka aye!

 

Mwaka wa 1963

Tulijishindia Uhuru

Bendera ya Mzungu iliteremshwa

Mwafrika alianza kujitawala

Tuliambiwa, ‘Harambee! Harambee!

Vuruteni mzigo.’

Tuliambiwa Fuata Nyayo!

Fungeni macho fuata Nyayo!

 

(Rap)

Machozi ya mKenya inagonga mchanga wa Afrika kama laana

Damu-victims kosana

Colonization aftermath ya urbanization

Matokeo ghetto kibao zenye homeless, landless

Merciless, visionless leaders

Kuendeleza nepotism, tribal clashes,capitalism

Division ya social classes

Division from Runda to Kibera, Kileleshwa to Dandora

Tulisahau rangi za bendera

History,haki na Ukweli

Swali. Mtumwa wa kiakili unaenda wapi kama umefunga macho?

Juu yako na vizazi vijavyo

Hurry mKenya

Kuamka au kutoamka

Kilio cha Mama Afrika

Kunajisiwa kisiasa.

 

Na bado twangoja wokovu

Twaangalia milimani

Twauliza Mwokozi wa nani

Twafaa kutazama kiooni

Kila mmoja ni kiongozi

Kila mmoja ni mwalimu

Kila mmoja ni mjenzi

Kila mmoja achukue madaraka

 

(Chorus)